Uoga Ni Kizuizi kikubwa Maishani Mwako
Karibu msomaji mpedwa kwenye makala aya... Soma kisha unipe wasia ama maoni yako hapo chini...
Je wajua kuwa watu wengi katika ulimwengu huu wamefeli maishani sio kwa kuwa ni wapumbavu_ lahasha bali wamekosa kuafikia mengi maishani kwa kuwa ni waoga_ wa kupindukia_.Hilo nalisema bila uoga wala tashwishi moyoni mwangu kwani katika fani hii ya uanahabari nimekutana na watu wa tabaka mbali mbali na kati ya hawa nikagundua kuwa kuna kikundi ambacho kimekumbwa_ na uoga wa mambo fulani.
Watu hawa ni wale ambao utotoni mwao walikumbwa na changamoto kadha wa kadha na hadi walipofi ka utu uzima, mizizi ya woga imekomaa na sasa uoga huu umekuwa ni kizuizi kikubwa katika maisha yao ya kila siku. Moja wapo wa mambo ambayo yametuathiri mnokatika utu uzima wetu ni uoga kuwa hatufai au hatutoshi mboga. Hali hii imetokana na kule kudunishwa na watu waliokuwa karibu nasi — wazazi ama hata marafi ki.
Sasa mambo mambo yamekuwa ya uoga mwingi maishani mwetu. Kwasabuka nilidadisi hapo mbeleni kuwa uoga ni adui , kupigana na uoga ni lazima. Chochote unachohofia kitazame kwa macho kizungumzie kwa sauti_ ya juu na ukieleze wazi kuwa kikukome. Njia mzuri ya kumaliza uoga maishani, ni wakati ule utajikubali ulivyo na pia kutizama kinachokukosesha usingizi kwa macho na kukichukulia hatua.
Baadhi ya watu ambao wamefaulu_ duniani kwa fani mbalimbali ni watu ambao walipiga moyo konde na kujua fi ka kuwa uoga upo lakini hawataangaziauoga bali wataangazia swala kubwa kuliko uoga. Pia waliangazia azma yao ya kutamani kufanikiwa , na kufunga milango na madirisha yote yaliokuwa yanaingisha uoga n hali ya mshikemshike.
Kwani hatima ya uoga ni kuishi maisha kana kwamba uko gerezani bali ni wewe mwenyewe uliyejitia huko. na ukafi cha ufunguo , ni nani atakakaye kukomboa? Ni wewe tu! Amua leo kuishi maisha ya ujasiri.Weka kifua mbele na uchague kuwa shujaa daima dawamu ukimwamini Mwenyezi mungu kwa hali yeyote maishani mwako. mfano utakuta kwamba kuna watu ambao hushindwa kutoa maoni yao mbele ya watu,_ kimoyomoyo wanadhana kuwa maoni yao hayafai au hata ni bure kabisa. Wengine nao hawawezi kudhubutu kuuliza swali kwani wanadhani kuwa maswali yao ni ya kipumbavu wengine nao wameshindwa kutumia talanta zao kwa uoga kuwa watapata kicheko na kuwa watafeli._ Haya maswala_ yanaashiria uoga na uoga huo ndio huwa kizingiti kikubwa kwa watu wengi.
Kuna aina mbali mbali za uoga ambao huathiri watu — watu wengi huwa na uoga wa kukataliwa (rejection) hii inamaanisha kuwa afadhali asije akaomba kazi au hata kumchumbia mtu iliasijen akakataliwa. Uoga huo humfanya mtu aishi maisha ya upweke na_ kuhisi kana kwamba yuko jela. Uoga mwengine ni ule wa kukataa mabadiliko. Kwa mfano mabadiliko maishani huja wakati mmoja au mwengine na kuna watu ambao hawapendi mabadiliko —yawe ni ya kikazi, serikalini au hata maisha yao yenyewe.
Na kwa hio wanapokumbanaa mabadiliko wao huona kana kwamba dunia inakwisha na wakati mwingi wao hutoroka majukumu waliopewa bila sababu makhsusi. Uoga wa kuwachwa mpweke. Watu wengine hawawezi kukata kauli maishani pasipo maoni ya watu wengine kwani wanaogopa kuwa pekee yao — yaani wao wanasubiri maoni ya wenzao ili waamue mwelekeo wao
Aina ya uoga_ huu husababisha mtu kutopiga hatua zozozote_ maishani na wanahisi kana kwamba wanazunguka zunguka huku na kule bila mwelekeo. Usifikiri kuwa ulimwengu wote unaweza kukupenda na kukubali — usijawe na uoga kwa kuwa kunao watu ambao wahakupendi, wala kukuthamini. Ni kawaida kupendwa na kuchukiwa — kwamba kuna watu ambao wana uoga kuwa hawatapendeka licha ya juhudi zao, na kwa hiyo wanaingilia tabia za kujipendekeza kwa watu.
Huo ni uoga ,na uoga huu unamfanya mtu kuwa anaishi maisha ya kuigiza na wala sio kwa uhalisia wake. Ukitaka kujua iwapo unaadhirika na uoga angalia hatua unazochukua kila siku kwani ikiwa unang’ang’ana_ kila kuchao kuepuka uoga — basi
umezingirwa nao.

Comments
Post a Comment